Watendaji
Mpangilio mzuri ndiyo msingi wa mambo yote.
Watendaji ndiyo wawakilishi wa utamaduni na mpangilio, wakitumia uelewaji wao wa mambo yanayofaa, yasiyofaa na yanayokubalika katika jamii ili kuleta familia na jamii pamoja. Wakiwa na maadili ya uaminifu, wakfu na heshima, watu wenye aina hii ya nafsi ya Watendaji wanathaminiwa kwa ushauri na mwongozo wao wazi, na wana furaha kuongoza njia wakati mgumu. Wakijivunia kuwaleta watu pamoja, Watendaji huchukua jukumu la waratibu wa jamii, wakijitahidi kuleta watu wote pamoja kusherehekea matukio muhimu ya jamii, au kulinda maadili ya kitamaduni yanayoshikilia familia na jamii pamoja.
Mtu Yeyote Mwenye Ujasiri Hupigania Anachoamini Kinafaa...
Mahitaji ya viongozi kama hawa yako juu katika jamii za kidemokrasia, na wakijumuisha 11% na kuendelea ya idadi ya watu, si ajabu kwamba viongozi wengi maarufu wa kisiasa na biashara duniani kote ni Watendaji. Watetezi wakubwa wa sheria na mamlaka ambayo lazima yafanyiwe kazi, Watendaji huongoza kwa mfano, wakionyesha imani na uaminifu wenye sababu, na kukataa kabisa uzembe na uongo, hasa kazini. Ikiwa mtu yeyote atasema kwamba kazi ngumu ya mikono ndiyo njia bora ya kuimarisha tabia, ni mtu mwenye nafsi hii ya Watendaji.
Watendaji wanafahamu mazingira yao na huishi katika dunia ya ukweli wazi unaoweza kuthibitishwa – uhakika wa ujuzi wao inamaanisha kwamba hata wakikumbana na upinzani mkubwa, wanakwamilia maadili yao na kusukuma dira wazi ya kinachokubalika na kisichokubalika. Maoni yao si maneno matupu, kwani Watendaji huwa tayari kujihusisha katika miradi migumu zaidi, wakiboresha mipango ya kazi na kupanga maelezo wanapofanya kazi, wakifanya hata kazi ngumu zaidi kuonekana zikiwa rahisi na za kutekelezeka.
Hata hivyo, Watendaji huwa hawafanyi kazi peke yao, na wanatarajia uaminifu wao na maadili yao ya kazi yaigwe – watu wenye nafsi ya aina hii hutimiza ahadi zao, na ikiwa wabia au wasaidizi wao watahatarisha ahadi hizo kwa kutokuwa na uwezo wa kuzitekeleza au uzembe, au mbaya zaidi, udanganyifu, huwatasita kuonyesha hasira zao. Jambo hili linaweza kuwapa sifa kama watu wasio rahisi kubadilika, lakini sio kwa sababu Watendaji ni wakaidi kidhalimu, lakini kwa sababu wanaamini kwa kweli kwamba maadili haya ndiyo hufanya jamii kuendelea vizuri.
...Lakini Bado Wazuri Zaidi Ni Wale Wanakubali Wanapokosea
Changamoto kuu kwa watu wenye nafsi hii ya Watendaji ni kukubali kwamba sio kila mtu anafuata njia sawa nao au kuchangia namna sawa nao. Kiongozi mzuri hutambua uwezo wa watu binafsi, pamoja na uwezo wa kundi, na husaidia kuleta dhana hizo tofauti kwenye jukwaa moja. Kwa njia hiyo, Watendaji huwa na ukweli wote, na wanaweza kuongoza upande unaowafaa watu wote.