Waasisi
Iko peke yake juu, na ikiwa moja ya aina nadra zaidi ya nafsi na yenye uwezo zaidi wa kimkakati, Waasisi wanajua hivyo vizuri. Waasisi wanajumuisha asilimia mbili tu za idadi ya watu, na wanawake wa aina hii ya nafsi huwa nadra sana, wakijumuisha 0.8% ya idadi ya watu – mara nyingi huwa ni changamoto kwao kupata watu wenye fikra sawa na wao wanaoweza kushindana na umaizi wao na ujanja wao kama wa sataranji. Watu wenye aina hii ya nafsi ya Uasisi ni wabunifu lakini wenye kufanya uamuzi, wenye kutaka makuu lakini wasiri, wadadisi wa kushangaza, lakini hawatumii nguvu zao vibaya.
Hakuna Kitu Kinaweza Kusimamisha Mtazamo Mzuri Kutimiza Lengo Lake
Wakiwa na tamaa asili ya kupata ujuzi inayojionyesha yenyewe mapema maishani, Waasisi mara nyingi hupewa jina la “mbukuzi” wakiwa watoto. Ingawa jina hili huenda likakusudiwa kama matusi kutoka kwa watu wa rika lao, huenda wakajitambulisha zaidi na jina hilo na hata hujivunia jina hilo, wakifurahia ujuzi wao mpana na wa kina. Waasisi hufurahia kushiriki wanachojua pia, wakijiamini katika ustadi wao wa mada walizochagua, lakini sifa hizi zinapendelea kubuni na kutekeleza mpango mzuri katika nyanja zao badala ya kushiriki maoni kuhusu vikengeushi “visivyowavutia” kama vile porojo.
Huna haki ya maoni yako. Una haki ya maoni yako unayoyaelewa. Hakuna mtu ana haki ya kuwa mjinga.
Likiwa fumbo kwa watazamaji wengi, Waasisi wanaweza kuishi kwa kutazama migongano ambayo hata hivyo ina maana kamilifu – angalau kutoka kwenye mtazamo wa urazini. Kwa mfano, Waasisi huwa wadhanifu wasiofikiria na wabeuzi wakali kabisa kwa wakati mmoja, mgongano unaoonekana kama usiowezekana. Lakini hii ni kwa sababu watu wenye aina ya nafsi ya Uasisi huamini kwamba kwa juhudi, umaizi na uzingatiaji, hakuna kitu ambacho hakiwezekani, huku kwa wakati huo huo wanaamini kwamba watu ni wazembe sana, wasioona mbali au wanaojitumikia kutimiza matokeo hayo mazuri. Lakini mtazamo huo wa ubeuzi wa ukweli hauwezi kumzuia Muasisi anayetaka kutimiza matokeo wanayoamini kuwa muhimu.
Kwa Mambo ya Kanuni, Kuwa Imara Kama Mwamba
Waasisi hutoa imani ya kujiamini na hali ya siri, na mitazamo yao ya ufahamu, dhana asili na mantiki ngumu huwawezesha kulazimisha mabadiliko kupitia utashi mtupu na nguvu ya nafsi. Wakati mwingine itaonekana kama Waasisi wanapendekeza uundaji upya wa kila dhana na mfumo wanaoshirikiana nao, wakitumia ukamilifu na hata uadilifu katika kazi hii. Mtu yeyote ambaye hana kipaji cha kushindana na taratibu za Waasisi, au vibaya zaidi, anayekosa kuona mawazo yao, huenda akapoteza heshima zao mara moja na kabisa.
Hii haifai kueleweka vibaya kama utendaji kwa ghafla bila mpangilio – Waasisi watajikakamua kuendelea kuwa mantiki bila kujali vile lengo la mwisho linavutia, na kila dhana, iwe imetoka ndani au kutoka nje, lazima ipite kichujio kikali na kinachotumika wakati wote cha “Je, dhana hii itafanya kazi?”. Utaratibu huu unatumika wakati wote, kwa mambo yote na watu wote, na hapa ndipo aina za nafsi ya Waasisi hujipata mashakani.
Mtu Hufikiria Zaidi Anaposafiri Peke Yake
Waasisi wanabobea na wana imani katika sekta za ujuzi walizochukua muda kuzielewa, lakini kwa bahati mbaya kuna uwezekano mkataba wa kijamii usiwe moja ya mada hizo. Uongo usiodhuru na majadiliano madogo ni magumu kwa sababu ni ya aina ya nafsi inyotamani ukweli na undani, lakini Waasisi huenda wakaona kongamano zingine za kijamii zikiwa za kipumbavu. Jambo la kinyume, mara nyingi huwa vizuri wasalie mahali wanapohisi vizuri – mbali na mwangaza – ambapo imani asili iliyo katika Waasisi wanapofanya kazi inaweza kutumika kama minara ya kibinafsi, ikivutia watu, kimapenzi au vinginevyo, wenye tabia na matakwa sawa.
Waasisi wanafafanuliwa na mwelekeo wao wa kuishi maisha kama ni ubao mkubwa wa sataranji, wakisogeza vipande vya sataranji mara kwa mara kwa uzingatiaji na umaizi, wakitathmini mbinu, mikakati na mipango mipya ya dharura, wakiwashinda watu wa rika lao ili kudumisha udhibiti wa hali huku wakizidisha uhuru wao wa kusogea. Hii haimaanishi kupendekeza kwamba Waasisi hutenda bila fikra, lakini kwa aina zingine nyingi, chuki ya Waasisi ya kutenda kutokana na mihemuko inaweza kuonekana kwa namna hiyo, na inafafanua kwa nini watu wabaya wa kitamthiliya (na mashujaa walioeleweka vibaya) hubainishwa katika aina hii ya nafsi.